Kikao cha Mapitio ya utekelezaji wa Mradi wa Uendelezaji wa Bonde la Msimbazi kufahamu hatua zilizofikiwa katika utekelezaji (progress implementation of the project) kinachofanyika katika ukumbi wa Serengeti Millenium Tower, Kijitonyama Dar es Salaam.

Serikali ya Tanzania, kupitia Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kwa kushirikiana na Wizara ya Ujenzi, inatekeleza Mradi wa Uendelezaji wa Bonde la Msimbazi kwa kiasi cha dola za Marekani milioni 260, ambapo kiasi cha dola milioni 200 ni mkopo nafuu kutoka Benki ya Dunia, dola milioni 30 ufadhili wa Serikali ya Uholanzi na dola milioni 30 ni mkopo kutoka Serikali ya Hispania.

Aidha, Wakala ya Barabara za Vijijini na Mjini Tanzania (TARURA) na Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) ndiyo watekelezaji wa Mradi wa Uendelezaji wa Bonde la Msimbazi kwa niaba ya wizara husika.

Leave A Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *